top of page

Kujitolea

Mtoto Mchoraji ni kwa ajili ya Sanaa na elimu, hata hivyo tunakaribisha wasanii, wanafunzi, waalimu, na mtu mmoja mmoja wa rika na madaraja yote ulimwenguni kote kujihusisha. Kuhusika kwako kunaweza ni kwa kupitia eneo lako la sanaa, shule, jamii, vikundi vya michezo na sanaa, mashirika, vilabu, vilabu vya kijamii na kidini, mahali pa ajira, au kama mtu binafsi.

Zifuatazo ni njia kadhaa ambazo watu walitumia kusaidia hapo awali:

  • Andaa kampeni za uchangishaji wa pesa shuleni, kilabuni, au katika jamii yako.

  • Kueneza habari za shughuli na uhitaji wa MM kupitia mitandao ya kijamii.

  • Tengeneza Ushirikiano wa Udhamini na marafiki, familia, wanafunzi wenzako, au majirani kudhamini mwanafunzi mmoja au zaidi.

  • Panga kikundi, wanafunzi, msanii, familia au watu kibinafsi kwa ajili safari za kimasoma ya sanaa, semina, na tembelea MM

  • Fanya mazungumzo kupitia Skype na wanachama wa MM / wanafunzi kupitia shule au kilabu yako.

  • Andaa hafla za kimisaada kwa kuunga mkono MM

  • Kupanga maonyesho, ya wanafunzi, na majukwaa ya vijana ya kubadilishana sanaa.

  • Kujitolea nchini Tanzania, kufundisha Kiingereza, Sanaa, na ustadi wa Kompyuta.

  • Kualika MM kwenye matamasha mbalimbali, na maonyesho ya sanaa.

  • Kufadhili Kijana au Mtoto.

Safiri na Mtoto Mchoraji

 

Mtoto Mchoraji ipo tayari kuongoza kikundi cha wanafunzi, familia kwa safari ya kimuingiliano wa kiutamaduni / huduma za safari  kuzunguka Tanzania wakati wa likizo, utafiti au ziara za kimasomo.

 

  • Fanya kazi na Wasichana na Wanawake ili kuwezesha Jamii.

 

  • Tembelea shule za bweni za wasichana na vituo vya watoto yatima.

 

  • Tambua historia, utamaduni, maisha, na mtindo wa maisha wa watu wa Bagamoyo, onana na wasanaa wa ndani fahamu jinsi wanavyofanya kazi, nunua, pata uzoefu kwa kufanya nao kazi.

 

  • Pumzika kwenye pwani ya Bagamoyo, tembelea soko huru (Soko la Jumatatu) ununue chakula safi na vitu vya kitanzania, nenda safari katika ya kitaifa iliyo karibu (Hifadhi ya Kitaifa ya Saadan), fanya safari ya mashua na ogelea kwa chombo cha kupumulia kwenye Bahari la Hindi. Picha Bure.

CHUNGUZA|ELIMISHA|INUA|ENDELEZA|BADILI

2020 Inamilikiwa na Shirika la Mtoto Mchoraji.

bottom of page