top of page

JINSI GANI UNAWEZA KUSAIDIA KITUO

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Bagamoyo, Tanzania, tafadhali tembelea kituo hicho! Tunakaribisha wageni, wanaojitolea, na marafiki wakati wote! Tafadhali fikiria kukaa na sisi kujitolea kwa muda fulani. Tunafurahi kupata watu wa kujitolea kusaidia kufundisha Kiingereza, kusoma, kuandika, hesabu za kimsingi, sanaa na kusaidia kazi ya shule. Ikiwa wewe ni msanii wa (Sanaa za mikono au Maonesho), tafadhali njoo ushiriki talanta zako na watoto na walimu. Tunafurahi, tupotayari kukusaidia kutafuta malazi salama, starehe, na ya bei nafuu kwa makazi yako.


Wakati umetembelea, unaweza kuchukua muda kuvinjari kazi zetu za sanaa za mikono, vito vya mapambo, na kadi ambazo zinapatikana na kuuzwa. Pesa inayopatikana kutokana na vitu hivi  kusaidia kituo, watoto na vijana ambao tunafanya nao kazi. Ununuzi wowote, mkubwa au mdogo, unathaminiwa sana. Ikiwa unatafuta kitu fulani maalum au binafsi, zungumza na walimu, ni wasanii wenye  vipaji watafurahi kuunda kitu maalum kwa ajili yako au familia yako na marafiki wa nyumbani.
 

Drawing1.JPG
Ngoma ya Magongo/Bugobogobo/dance/Dry face/Mtoto Mchoraji/Local Volunteer/Amsha Tucheze
Get Involved/Volunteer@mm
Dance workshop/friend Class/Norway Dance teacher/Volunteer teacher/movement of dance/mtoto mchoraji/mm/art/center

KAMA HAUTOWEZA KUTEMBELEA......

Ikiwa hauwezi kufanya safari ya kwenda Tanzania kwa wakati huu, kuna njia zingine nyingi ambazo unaweza kusaidia kituo hicho.
 

Machaguo ya vito vya mapambo na michoro inapatikana kwa ununuzi na vinaweza kufikishwa kwa anuwani ya nchi.  Ikiwa una nia ya kununua kitu kutoka kituo, tafadhali wasiliana nasi na tunaweza kukutumia picha ya vitu ambazo zinapatikana kwa wakati huo.

 

neckless.jpg
notebook.jpg
masai 1-1.JPG
Tunafurahi pia tunakubali michango ya kifedha na michango ya vitu vingine kusaidia shughuli zetu watoto na vijana!
Mchango wowote ni muhimu na huleta mabadiliko kwa Watoto hawa. 
Bonyeza hapo kwenye moyo  wa kijani,uwasiliane nasi ili ujue njia zingine za kuweza kusaidia kituo!

CHUNGUZA|ELIMISHA|INUA|ENDELEZA|BADILI

2020 Inamilikiwa na Shirika la Mtoto Mchoraji.

bottom of page