Kwanini Mtoto Mchoraji (MM)
Kuita kituo Mtoto Mchoraji (Drawing Child) haimaanishi tunashughulika na kuchora pekee.
Kuchora imetumika kama neno la jumla kwa sababu ndio msingi wa aina zote za sanaa. Inaweza kufafanuliwa kama uwakilishi wa takwimu za kawaida zinazoandaliwa na hatua inayoweza kusisitiza na kufafanua sura ya kitu, ishara, hisia, au wazo.
Mtoto ni kama ncha ya kitu kinachojongea kutoka utotoni kuelekea utu uzima, akichora njia ya maisha yake ya baadaye. Wanachohitaji ni msaada wetu ili waweze kuchora njia nzuri ya maisha.
Ndio sababu tunafundisha, kuunga mkono, kutunza, na kuwapa stadi.
Watoto huzaliwa na talanta za kisanii na wanapata msukumo na maono tofauti kulingana na shughuli zao za kila siku.
Vipaji hivi hufanya iwe rahisi kwao kujifunza na kujiweka huru kiakili na kimwili. Wanaweza kutumia uwezo wao kujielezea kwa wengine kupitia shughuli za sanaa.
Watoto wengine wengi kutoka kitongojini huja kwenye kituo kutazama watoto na vijana wa Mtoto Mchoraji wakiunda sanaa, wakijifunza kucheza na kupiga ngoma. Watoto hao, ambao hawana hasa cha kufanya, huathiriwa pia kwa sababu uhamasishwa na kuburudishwa. Siku moja, watoto na vijana waliopo katika kituo hiki watakuwa na uwezo wa kuelimisha na kuwapa wengine yote waliyojifunza.
Hii inafanya Mtoto Mchoraji kuwa endelevu na husababisha matokeo kubwa katika jamii.