top of page
WASIFU WA WATOTO
Upo mahali sahihi tafadhali tunaomba muda wako tazama wasifu wa mtoto wetu, uwafahamu. Usisite kuwasiliana nasi wakati wowote unapohitaji kututembelea/kusaidia, kundi, au mtu mmoja mmoja. Karibu
BRIANA NICKSON (8)
Watu wengi wananiita '' ANA '', mimi ni mwanafunzi wa darasa la 1. Nilijiunga kwenye Kituo cha Mtoto Mchoraji nilipokuwa na umri wa miaka 5, bado najifunza KUJIPINDA VIUNGO VYA MWILI (kubadilika kwa mwili), Kucheza Ngoma, Uchoraji, na Ustadi wa Maisha. Tayari nimeshashiriki na kufanya maonesho kwenye Tamasha kubwa la Sanaa nikiwa na umri mdogo kwa msaada wa Mtoto Mchoraji. Ninajivunia hilo.
ASNATH ALLY (9)
Mimi ni mwanafunzi wa darasa la III. Wakati nilipokuwa na umri wa miaka 5 bibi yangu alinipeleka kwenye kituo cha Mtoto Mchoraji kujifunza KUPINDA VIUNGO VYA MWILI (kubadilika kwa mwili), Uchoraji, Kucheza ngoma na Ustadi wa Maisha. Mwaka 2019 nillifanya onesho langu la kwanza kwenye Tamasha la Sanaa la Bagamoyo.
PETER JOSEPH (10)
Mimi ni mwanafunzi wa darasa la tatu. Bado ni mwanafunzi mpya katika Kituo cha Mtoto Mchoraji najifunza KUJIPINDA VIUNGO VYA MWILI (kubadilika kwa mwili), Kuchora, na Ustadi wa Maisha.
EMMANUEL BARAKA (10)
Unaweza kuniita Imma badala yake, ninasoma shule ya awali, pia ni mtoto mpya katika Kituo cha Mtoto Mchoraji. Natumai walimu wangu wataniunga mkono na kunifundisha mengi. Tafadhali naomba msaada wenu
SHEILA RAJABU (11)
Nilijiunga katika Kituo cha Mtoto Mchoraji nikiwa umri mdogo sana, mimi ni Mcheza ngoma, na Mpinda viungo vya mwili (kubadilika kwa Mwili), hadi sasa bado ninajifunza ujuzi mpya katika sanaa ya mikono na Ustadi wa Maisha. Mbali na hayo mimi ni mwanafunzi wa shule ya msingi darasa la IV. Ninaishi kijiji cha Ukuni hapa katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo.
SUZANA PETER (11)
Unaweza kuniita '' SUZY '', mimi ndiye mtoto wa pekee katika familia yetu, mama yangu aliaga dunia nilipokuwa na umri wa mwaka 1. Kwenye Kituo cha Mtoto Mchoraji ninajifunza Yoga (kubadilika kwa Mwili), Kucheza Ngoma, Kuchora, na Ustadi wa Maisha. Nimeweza kushiriki kwenye Tamasha kubwa la Sanaa kwa msaada na hudumu ya Mtoto Mchoraji katika umri mdogo. Ninajivunia hilo.
JUMA FIKIRI (13)
Mimi ni mwanafunzi wa darasa la 5. Ninapenda sanaa, mpira wa miguu na uvuvi. Katika Kituo cha Mtoto Mchoraji ninasoma Kurusha kofia,, KUPINDA VIUNGO VYA MWILI(kubadilika kwa Mwili), Kucheza Ngoma, Uchoraji, na Ustadi wa Maisha. Tayari nimeshashiriki kwenye matamasha na maonesha mbalimbali ya sanaa kupitia kituo cha Mtoto Mchoraji katika umri mdogo sana.
ZAWADI NICHORUS
Kila Agosti 5 ni siku yangu ya kuzaliwa, mimi ni mwanafunzi wa shule ya msingi. Nilijiunga na Kituo cha Mtoto Mchoraji nilipokuwa daraja la 3, bado najifunza Rola bola (kusawazisha), Kucheza Ngoma, Uchoraji, na mbinu za Maisha. Ninataka pia kujifunza ujuzi mwingine katika sanaa ya maonesho na mikono.
HUSNA MBARAKA (16)
Mimi ni mcheza ngoma. Ingawa wazazi wangu wanataka nizingatie zaidi masomo tangu nilipoingia shule ya sekondari kwa hivyo sifanyi uchezaji sana siku hizi. Nilianza kujifunza Mtoto Mchoraji nilipokuwa na umri wa miaka 5, nilishafanya maonesho kwenye hafla tofauti
CELINA GEORGE (16)
Nilianza kuwa mtoto wa kituo cha Mtoto Mchoraji mnamo 2018. Kwa kawaida najiunga na watoto wenzangu kwa mafunzo ya sanaa siku za mwisho wa juma kwa sababu mimi naishi takribani kilomita 24 kutoka kituo kilipo. Ninakosa mafunzo / mazoezi ya siku za wiki nyingi, na majuma kadhaa kwa sababu inanibidi niwahi kurudi nyumbani. Uwa nafanya hivyo kwa shule pia. Natamani ningeweza kukaa karibu ya shule au kituo cha sanaa, kama watoto wengine ambao wanaishi karibu.
ZAWADI OMARY (16)
Mimi ni mwanafunzi wa shule ya sekondari. Ninajihisi mwenye bahati sana kwani naweza kushiriki katika programu za utamaduni na michezo ya shule kwa sababu ninajifunza mengi toka Mtoto Mchoraji. Sasa naweza kufanya urushaji vitenesi, kucheza ngoma, na najua Ujuzi kidogo wa Maisha.
HIDAYA RAJABU (16)
Ninaishi karibu na Kituo cha Mtoto Mchoraji kwa hivyo ni rahisi kwangu kuongeza muda na kufanya mazoezi zaidi kila baada ya kipindi cha mafunzo. Kupitia Mtoto Mchoraji mimi nimekuwa Mchezaji na Mpindaji Viungo vya mwili.
GRACE SALUM (16)
Ninaishi Ukuni shule Bagamoyo, nimejiunga Mtoto Mchoraji nikiwa na umri wa miaka 5 baada yakuwaona wametembelea shuleni kwetu kwa ajili ya mpango wa Ubadilishanaji wa Sanaa na Utamaduni, nilivutiwa na kile walichokuwa wakifanya, nilishangazwa zaidi kuwaona marafiki zangu wa shule tayari wameshajiunga. Nilimuomba mama yangu na akaenda kuniandikisha. Tangu wakati huo mimi ni sehemu ya MM.
MTEPA MROPE (17)
Kituo cha Mtoto Mchoraji ni nyumbani. Ni mahali salama kabisa kwangu, mara kwa mara hutumia wakati wangu wa mapumziko huko Mtoto. Kupitia mahali hapa pa sanaa, nimejifunza kucheza, Kuchora, kurusha, sanaa za mikono, kutembea kwa baisikeli ya gurudumu moja, Kupiga na kutengeneza ngoma pia kupinduka kwa mtindo wa sarakasi.
MWANABARAKA HAJI (19)
Unaweza kuniita '' MWANA ''. Mimi ni mwanafunzi wa kiwango cha O niliyejiunga katika Kituo cha Mtoto Mchoraji nilipokuwa shule ya msingi. Ninafanya Upindaji wa mwili (Mwili wa kubadilika / Yoga), nacheza Kitambaa na ngoma. Tangu nijiunge na Mtoto nimepata marafiki wengi ndani na nje ya Tanzania. Ninapenda watu kwa sababu sisi ni wamoja.
FAUSTINE MAYUNGA (20)
Mimi nacheza ngoma na kurusha kofia, tangu nilipojiunga katika Kituo cha Mtoto Mchoraji ninajisikia salama na fahari. Nimejifunza mambo mengi kupitia Sanaa na Elimu, mbali na kwamba walinifundisha ustadi wa maisha na maisha kwa ujumla sasa nimegundua kuwa wanadamu wote ni sawa, na Kushiriki ni Kujali.
SUDI JUMA (20)
Marafiki zangu kuniita SUDY BROWN, pia mimi ni mwanafunzi wa kiwango cha O. Nilijiunga katika Kituo cha Mtoto Mchoraji mwaka 2019, bado anasoma Uchezaji, Kuchora, kutengeneza mapambo ya vito, Kupiga na kutengeneza ngoma, Rola Bola, Kurusha kofia, na Stadi za Maisha.
MUDHIHIR FERUZI (17)
Mimi ni pacha, kaka yangu pia anapenda sanaa. Anaweza kufanya kile mimi ninachofanya (Kucheza ngoma na kubinjuka/sarakasi) mama yetu ni msanii (Mchezaji) alituambia kwamba babu yetu alikuwa msanii pia, (mwanamuziki) lakini baba yetu ni fundi. Unaweza kuniita PARA jina linalojulikana sana kwa familia yangu, marafiki na wanafunzi wenzangu. Ninafurahi kuwa mmoja wa watoto wa Mtoto Mchoraji.
bottom of page